Kibonde kuzikwa makaburi ya Kinondoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Mar 2019
Kibonde kuzikwa makaburi ya Kinondoni

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM Ephraim Kibonde unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Kibonde ambaye pia alikuwa mtangazaji/mchambuzi wa soka kin'gamuzi cha DSTV kwa lugha ya kiswahili, alifariki mkoani Mwanza juzi katika Hospitali ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mfupi

Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Africana ambapo jana Waziri Mkuu Mh Majaliwa Kassim alifika kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli

Msemaji wa familia, Saudiri Mwakaje alisema mwili utafika nyumbani Mbezi Africana saa 4:30 asubuhi kutoka Hospitali ya Lugalo, saa sita watu watapata chakula cha mchana ikifuatiwa na ibada na kuaga baada ya hapo safari ya makaburini itaanza.

Kifo cha Kibonde kimewashtua wengi kutokana na ukweli kwamba siku tatu kabla ya umauti kumfika alikuwa wilayani Bukoba akisimamia shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media marehemu Ruge Mutahaba aliyefariki Februari 26 Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu

Kibonde alisimamia hafla ya kuagwa mwili wa Ruge iliyofanyika jijini Dar es salaam na baadae kusimamia hafla ya maziko wilayani Bukoba

Alianza kuugua wakati shughuli za maziko ya Ruge zikiendelea

Taarifa iliyotolewa na familia imeeleza marehemu alibainika kuwa na uvimbe tumboni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’