Msafara wa kikosi cha Simba umewasili salama mji wa Bechar tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura utakaopigwa kesho Jumamosi katika dimba la Agosti 20 1955
Simba ilifikia mji wa Algiers ambayo ndiyo Makao Makuu ya Algeria na kufanya mazoezi kwa siku mbili kabla ya leo asubuhi kuelekea mji huo wa Bechar ambako ndiko yalipo Makao ya klabu ya JS Saoura
Simba imetumia usafiri wa Ndege kutoka Algiers mpaka Bechar kwani kuna umbali mrefu wa takribani kilomita 1000 baina ya miji hiyo
Leo Simba inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Agosti 20 ambao utatumika katika mchezo wa kesho


ADVERTISE HERE