Kocha JS Saoura apagawa, kisa Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Mar 2019
Kocha JS Saoura apagawa, kisa Kagere

JS Saoura imeingia mchecheto baada ya kuwasili kikosi cha Simba nchini Algeria tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa keshokutwa Jumamosi katika dimba la Agosti 20 1955

Karim Zaoui ndiye kocha Mkuu wa timu hiyo kwa sasa ambapo alichukua nafasi ya Nabil Neghiz aliyetimuliwa baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa

Mtandao wa JS Saoura umeripoti kuwa kocha huyo amewatahadharisha mabeki wa timu hiyo kuwa wasipomchunga Meddie Kagere wanaweza kupoteza mchezo wa keshokutwa

Kagere aliwafunga mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza

Mchezo huo baina ya timu hizo utapigwa Jumamosi hii, mjini Bechar, utachezeshwa na waamuzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Waamuzi hao ni Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayepuliza kipyenga na mshika kibendera namba moja, Olivier Safari Kabene, wakati mshika kibendera wa pili, Soulaimane Amaldine anatokea Comoro.

Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, huku Al Ahly ambayo wikiendi hii watakuwa ugenini kwa AS Vita mjini Kinshasa, ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zao saba.

JS Saoura, yenye mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu, inashika nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja na Simba SC na yenyewe ikiizidi pointi moja AS Vita inayoshika mkia.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’