Kufuatia taarifa ya kufungwa uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex, Simba na vilabu vingine vya jijini Dar es salaam vimearifiwa kutafuta viwanja kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani
Viwanja hivyo vinatarajiwa kufungwa March 24 kufanyiwa ukarabati tayari kwa kutumika kwenye fainali za michuano ya vijana ya AFCON U17 itakayofanyika nchini kuanzia April 14-28 Tanzania ikiwa mwenyeji
Uongozi wa klabu ya Simba umependekeza kutumia uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani kwenye ligi wakati uwanja wa Taifa utakapofungwa
Tayari sehemu ya kuchezea ya uwanja huo imeanza kufanyiwa ukarabati ili kuwa tayari
Hata hivyo baadhi ya wadau wamekosoa uamuzi wa Simba kuchagua uwanja huo ambao 'mandhari' yake haiendani na falsafa ya soka la Simba la pasi fupi fupi
Wengi wamependekeza uwanja wa Samora wa mkoani Iringa au hata uwanja wa CCM Kirumba ambao inadaiwa klabu Yanga ndio itakaotumia
Azam Fc pia itaelekea jijini Mwanza kwenye uwanja wa Nyamagana