Wekundu wa Msimbazi, Simba wamepangwa kundi moja na Azam FC katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 30, 2017.
Simba imepangwa kundi A sambamba na Azam FC, URA, Jamhuri na Taifa Jang'ombe.
Azam na Simba zilikutana kwenye mchezo wa fainali mapema mwaka huu na Azam kuibuka na ushindi uliowezesha kutwaa taji la michuano hiyo mahsusi kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kundi A ndilo linatazamiwa kuwa na ushindani mkali ukilinganisha kundi B ambalo imepangwa klabu ya Yanga sambama na timu za Zimamoto, Mlandege, Shaba na JKU.

ADVERTISE HERE