Rais Magufuli aagiza waliomteka Mo wafikishwe Mahakamani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Mar 2019
Rais Magufuli aagiza waliomteka Mo wafikishwe Mahakamani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ameshangazwa na ukimya wa Jeshi la Polisi kufuatia tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara na Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo'

Akizungumza jijini Dar es salaam leo wakati wa zoezi la kuwaapisha Makamishna wa juu wa jeshi la Polisi pamoja na Mawaziri wapya wawili akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria na Dkt Agustine Mahiga pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi, Rais Magufuli amehoji ni kwa nini mpaka leo wahusika hawajafikishwa Mahakamani

"Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa," amesema Rais Magufuli

"Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa sawa", ameongeza Rais Magufuli

Oktoba 2018, akiwa Jijini Dar es salaam mfanyabiashara Mohemed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana ambao walitajwa kuwa ni raia kutoka nje ya nchi lakini baadaye alipatikana maeneo ya Gymkhana Jiji Dar es salaam.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’