Kikosi cha Simba kimewasili salama jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Shinyanga ambapo jana kilipata ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United
Msafara wa kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliondoka Shinyanga jana jioni baada ya mchezo na kulala mkoani Mwanza ambapo leo asubuhi waliondoka kwa usafiri wa ndege kurejea jijini Dar es salaam
Baada ya kupata ushindi wa asilimia 100 katika michezo yake sita ya ligi iliyopita, Simba inajiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura
Mchezo huo utapigwa nchini Algeria Jumamosi, March 09 2019
Kama Simba itashinda mchezo huo na Vita Club ikashindwa kupata ushindi dhidi ya Al Ahly, Simba itakuwa imejihakikishia kutinga robo fainali ya michuano hiyo



ADVERTISE HERE