FT : Stand United 0-2 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Mar 2019
FT : Stand United 0-2 Simba

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameendeleza vipigo kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuifumua Stand United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga

Licha ya kufanikiwa kuizuia Simba isifunge kwenye dakika 45 za kipindi cha kwanza, Stand 'ilichemsha' katika kipindi cha pili Simba ikifunga mabao yake yote kwenye kipindi hicho

Nahodha John Bocco ndiye aliyekuwa shujaa wa kikosi cha Simba leo akifunga mabao yote mawili

Bocco aliitanguliza Simba kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 52 baada ya mlinzi wa Stand United kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Stand walionekana kupania mchezo huo, walijikuta wakiokota mpira kambani kwa mara ya pili kwenye dakika ya 66 mfungaji akiwa Bocco

Matokeo hayo yameendeleza rekodi ya ushindi mfululizo kwa Simba sasa ikiwa imeshinda michezo yote iliyocheza tangu kuanza kwa mwaka 2019

Bocco ameendelea kuwasogelea vinara wa mabao katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu baada ya kufikisha mabao tisa

Simba imefikisha alama 51 baada ya kushuka dimbani mara 20, iko nyuma ya Azam Fc kwa tofauti ya alama mbili tu. Azam Fc imecheza michezo sita zaidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’