Aussems apania kunyamazisha 'kelele' za Stand United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Mar 2019
Aussems apania kunyamazisha 'kelele' za Stand United

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake imefuata alama tatu mkoani Shinyanga hivyo iko tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kambarage

Simba iliweka kambi ya siku mbili mkoani Singida kabla ya kutua Shinyanga hapo jana

Aussems amesema anatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi lakini kama walivyofanya katika michezo iliyopita, lengo lao ni kuondoka na alama zote tatu

Juzi kocha wa Stand United Athuman Bilali 'Bilo' alitamba kuwa timu yake itaibuka na ushindi katika mchezo huo ambapo alisema Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo Ndanda Fc, Mwadui Fc na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu

"Tumewafuata Stand United, tunajua kila timu sasa inajiandaa kuonyesha ushindani itakapocheza na sisi, tunajua hilo, lakini mipango yangu ni kuhakikisha tunashinda mechi hii ya Jumapili, tuko tayari," alisema Aussems jana baada ya kutua mkoani Shinyanga

Jana jioni kikosi cha Simba kilijifua mkoani Shinyanga kujiandaa na mchezo huo ambao ushindi utazidi kuisogeza Simba kileleni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’