Straika wa ZESCO atua Msimbazi kujaribiwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
30 Nov 2017
Straika wa ZESCO atua Msimbazi kujaribiwa
Wekundu wa Msimbazi, Simba wapo mbioni kumalizana na mshambuliaji wa Zesco United, Zambia, Jonas Sakuwaha.

Sakuhawa amewasili kwa majaribio katika kikosi cha Simba ambacho kitaanza mazoezi Ijumaa na atakuwa chini ya uangalizi wa kocha msaidizi Mrundi Masoud Djuma

“Tumewaambia viongozi wasisajili mchezaji yoyote wa kigeni bila kumuona katika mazoezi na kama tutakuwa hatujaridhishwa na kiwango chake tutamuacha na tutahitaji mwingine na kama atapatikana aliyokuwa vizuri ndio tutawambia viongozi wamalizane nae,” alisema.

“Omog ataondoka na jukumu litabaki kwangu na tutakuwa tunawasiliana kwa kipindi chote ambacho hatakuwepo hapa ili kama atakuja asiwe na kazi kubwa ya kuanza kumuangalia upya wachezaji ambao watakuwa katika majaribio,” alisema Djuma.

“Sijamuona Sakuwaha lakini nimesikia kuwa tayari ameshaingia nchini lakini nitakuwa na taarifa zake rasmi baada ya siku ya Ijumaa nikishamuona katika mazoezi yetu,” alisema Meneja wa Simba, Richard Robert.

Sakuwaha alizaliwa Julai 22, 1983 katika Mji Kafue nchini Zambia anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati au pembeni na ni mzuri katika kufunga kokote ambapo kocha atampa nafasi ya kucheza.

Sakuhawa ni mchezaji mzoefu kwani amecheza kwa miaka tofauti Zesco United, Lorient ya Ufaransa, El Merreikh ya Sudan na TP Mazembe ya DR Congo.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →