Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa Machi mosi 2019 na utazikwa Bukoba, mkoani Kagera Jumatatu ijayo
Msemaji wa famili Annik Kashasha amesema taratibu za kuuleta mwili zinafanyika nchini Afrika Kusini ambako marehemu alifariki juzi wakati akiendelea na matibabu.
"Mwili wa marehemu utarejeshwa hapa nchini siku ya Ijumaa (Machi 1) na siku ya Jumapili (Machi 3) utasafirishwa kwenda Bukoba kwaajili ya mazishi," alisema Kashasha
Kifo cha Ruge kimewashtua Watanzania kutokana na mchango wake hasa katika kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao
Klabu ya Simba kupitia taarifa yake rasmi ilieleza kushitushwa na kifo cha Ruge kilichotokea usiku wa juzi nchini Afrika Kusini
