Chama 'awapotezea' wanaosema ameshuka kiwango

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Feb 2019
Chama 'awapotezea' wanaosema ameshuka kiwango

Baada ya kukosolewa sana kutokana na kucheza chini ya kiwango kwenye mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga uliopigwa Februari 16, kiungo Clatous Chama amesema ataendelea kujituma na kufanya vizuri kadiri ya uwezo wake huku akiwataka wale wanaomkosoa kwa kutofanya vizuri kwenye mchezo mmoja watambue kuwa yeye ni binadamu

Juzi Chama aliwajibu wakosoaji hao kwa kupachika mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-1 iliyopata Simba dhidi ya Lipuli Fc

"Hakuna mchezaji anayependa kucheza katika kiwango cha chini, kila siku mchezaji hujipanga kuonyesha kiwango cha juu, lakini mazingira na wakati uliopo huchangia kuonekana tofauti, hapa ni Afrika na si Ulaya, mimi bado ni Chama yule yule," amesema Chama

"Nashukuru napata ushirikiano kutoka kwa wachezaji na benchi la Ufundi, umoja wetu ndio unaotufanya tuzidi kufanya vizuri. Naamini tutaendelea kufanya vizuri na kutimiza lengo letu la kutetea ubingwa msimu huu"

Kikosi cha Simba kiliwasili mkoani Singida jana na kitajifua mkoani humo kwa siku mbili kabla ya kuelekea Shinyanga kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili, Marhc 03 2019 katika uwanja wa CCM Kambarage

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
57m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’