Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli Fc jana, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka mkoani Iringa leo kuianza safari ya Shinyanga
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema kabla ya kuelekea Shinyanga, kikosi kitaweka kambi ya siku mbili mkoani Singida
Baadae ndio wataelekea Shinyanga kuifuata Stand United tayari kwa mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumapili, March 03 2019
Rweyemamu amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri ambapo leo asubuhi walifanya mazoezi ya kuweka sawa miili baada ya mchezo wa jana
ADVERTISE HERE