Simba yasaka alama tatu muhimu dhidi ya Lipuli Fc leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Feb 2019
Simba yasaka alama tatu muhimu dhidi ya Lipuli Fc leo

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo jioni kinashuka uwanja wa Samora mkoani Iringa kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu

Simba iko mkoani Iringa tangu juzi ambapo jana jioni ilifanya mazoezi yake ya mwisho dimba la Samora kuelekea mchezo huo

Kocha Mkuu wa mabingwa hao watetezi Patrick Aussems amesema anafahamu mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ushindani uliopo baina ya timu hizo hata hivyo anaamini timu yake itaendeleza kasi yake ya ushindi

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu. Lakini tumejiandaa na ukizingatia tumefanya vizuri katika michezo iliyopita, tunataka kuliendeleza hilo na tupo tayari," amesema Aussems

Mchezo wa leo utakuwa wa nne kuzikutanisha Lipuli na Simba tangu Lipuli ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita

Michezo mitatu iliyopita ilimalizika kwa sare hivyo leo Simba ina kila sababu ya kuchukua alama zote tatu ili kuendelea kusogea kileleni mwa msimamo wa ligi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’