Simba yapiga hesabu kali Iringa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Feb 2019
Simba yapiga hesabu kali Iringa

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba tayari kiko mkoani Iringa ambapo kesho Jumanne kitashuka katika uwanja wa Samora kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa ligi Kuu

Simba yenye alama 45 baada ya kushuka dimbani mara 18 itakuwa na nafasi ya kuendelea kusogea kileleni mwa msimamo kama itafanikiwa kuibuka na ushindi

Simba inakaribia kabisa kuipiku Azam Fc iliyo nafasi ya pili ikiwa na alama 50, huku hesabu zikiwa kuiondoa Yanga yenye alama 61 kileleni

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anatambua mchezo wa kesho hautakuwa mwepesi kutokana na uimara wa kikosi cha Lipuli lakini hesabu zake ni kupata alama tatu

Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka suluhu ya bila ya kufungana

Lipuli inayonolewa na Selemani Matola, tangu ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita, haijapoteza mchezo dhidi ya Simba

Kikosi cha Simba leo kitajifua kwenye dimba la Samora kujiweka sawa tayari kwa mtanage huo wa kesho

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’