Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amefurahishwa na matokeo ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Azam Fc jana katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Aussems amesema licha ya ugumu wa ratiba, vijana wake wametimiza wajibu wao na kuiwezesha Simba kushinda michezo yote katika wiki ambayo ilikuwa ngumu kwao
Katika kipindi cha wiki mbili Simba imefanikiwa kushinda michezo dhidi ya Mwadui Fc, Al Ahly, Yanga, African Lyon na jana Azam Fc
"Tumepata ushindi dhidi ya timu bora leo," Aussems aliwaambia waandishi wa habari jana
"Tulihitaji alama tatu, tumezipata sasa tunaelekeza nguvu zetu kwa mchezo unaofuata"
Baada ya mchezo wa jana, mchezo unaofuata ni dhidi ya Lipuli Fc, utakaopigwa mkoani Iringa Jumanne ijayo, Februari 26 2019
ADVERTISE HERE