Luizio azuiwa kujiunga Singida United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Nov 2017
Luizio azuiwa kujiunga Singida United
Harakati za klabu ya Singida United ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi hawataki kumuachia.

Singida inamuhitaji Liuzio kwa ajili ya kuongezea nguvu kikosi chake kwenye mzunguko wa pili baada ya kurizishwa na kiwango chake.

Rafiki wa karibu wa Liuzio amesema, ni kweli Singida wanamuhitaji mchezaji huyo lakini Simba imeonyesha dalili zote kuwa haitaki kumuachia.

"Kweli Singida inamtaka, Liuzio lakini Simba wamegoma, hawataki kumtoa sasa sijui kwa nini wakati wenyewe hawampi nafasi kubwa ya kucheza. Bora wangemtoa akajaribu maisha mengine huko,"alisema.

Liuzio mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, klabu iliyomlea na kumuuza Zesco ya Zambia, alirudi nchini mwaka jana akasajiliwa kwa mkopo na Simba anayoichezea mpaka sasa.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
37m ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
1h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
1h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
4h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’