Uongozi wa Simba umeachana na mpango wa kumuuza winga wake machachari Shiza Kichuya baada ya kutoridhishwa na dau lililotolewa na klabu ya Misri iliyotaka kumnunua.
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Simba ameuthibitishia mtandao huu kuwa mpango wa kumuuza Kichuya umesitishwa kwa sasa labda timu hiyo inayomtaka iongeze dau.
Bila ya kutaja kiasi cha fedha ilizotaka Simba kuweza kumuachia Kichuya, kiongozi huyo amesema Simba itaweza kumuuza kama kiwango chao kitafikiwa.
Kichuya amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Simba.

ADVERTISE HERE