Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wanashuka dimba la Taifa kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi mzunguuko wa 28
Simba iliyoshinda michezo minne iliyopita katika mashindano yote, imepania kuendeleza wimbi hilo la ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa
Kocha Patrick Aussems amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo licha ya wachezaji wake kurejea jijini Dar es salaam juzi wakitokea mkoani Arusha
Aussems amesema mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kuwa Azam fc inaundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu. Lakini lengo lao ni kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa timu hizo kukutana kwenye ligi msimu huu.
Azam Fc ilishinda michezo yote miwili iliyozikutanisha timu hizo katika michuano ya Kagame na kombe la Mapinduzi
Msimu uliopita Simba ilifanikiwa kuondoka na alama nne dhidi ya Azam Fc ikishinda mchezo wa mzunguuko wa pili kwa bao 1-0.
Mfungaji wa bao hilo alikuwa Emmanuel Okwi ambaye leo atakuwepo kikosini baada ya kukosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano