Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amekuwa na kiwango kizuri akiendeleza moto wa kupachika mabao katika kila mchezo anaoshuka dimbani
Kagere amefichua kuwa kuna timu nyingi zinamuwania akajiunge nazo
Miongoni mwa timu hizo ni TP Mazembe ambayo hii haitakuwa mara ya kwanza kutaka huduma ya mshambuliaji huyo aliyetua Simba msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya
Juzi Kagere katika mahojiano na Redio Rwanda, alikiri kufuatwa na viongozi wa TP Mazembe na timu nyingine kutoka Uturuki
Hata hivyo mshambiliaji huyo mkongwe amesema kwa sasa akili yake yote iko Simba na kwa kuwa bado ana mkataba na mabingwa hao wa Tanzania Bara, ataondoka iwapo viongozi wake watamruhusu
ADVERTISE HERE