Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba, kesho watakuwa dimba la Taifa kuikabili Azam katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 28
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon juzi, Simba ilirejea jijini Dar es salaam jana na jioni ilijifua katika uwanja wa Boko Veterans
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kila mchezo wanahitaji alama tatu ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa
Katika mchezo wa kesho, washambuliaji Emmanuel Okwi na Meddie Kagere watarejea kikosini baada ya kukosa mchezo dhidi ya African Lyon kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Hata hivyo Simba huenda ikawakosa Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima ambao walishindwa kufanya mazoezi jana wakikabiliwa na majeraha
Baada ya kufungwa na Azam Fc kwenye michuano ya kombe la Kagame na Mapinduzi Cup, kikosi cha Simba kesho kitakuwa na nafasi ya kulipa kisasi kwa wauza 'ice cream' hao wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 50