Baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-0 mkoani Arusha jana, kikosi cha Simba kinarejea jijini Dar es salaam kuikabili Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa keshokutwa Ijumaa, Februari 22 2019
Azam Fc itakuwa mwenyeji wa mchezo huo
Simba inakabiliwa na mfululizo wa michezo ya ugenini kwenye mashindano yote kwani baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, itaelekea mkoani Iringa kuikabili Lipuli Fc Februari 26 2019.
Ikitoka Iringa itaelekea mkoani Shinyanga kuikabili Stand United March 03 2019 kisha kuelekea Nchini Algeria kuikabili JS Saoura kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya tano
Wiki moja baadae Simba itarejea uwanja wa Taifa kuikabili As Vita Club kwenye mchezo wa wa mwisho wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa