Aussems awapongeza wachezaji kwa ushindi dhidi ya African Lyon

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Feb 2019
Aussems awapongeza wachezaji kwa ushindi dhidi ya African Lyon

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa dimba la Sheikh Amri Abeid

Aussems amesema malengo ya kikosi chake ilikuwa ni kushinda mchezo huo, matokeo hayo yamempa faraja

Katika mchezo wa leo Simba ilitumia mipira mirefu zaidi kuliko ilivyozoeleka. Aussems amesema walilazimika kutumia mfumo huo kutokana na changamoto ya uwanja

"Muhimu zaidi ni tumepata alama tatu. Tulijua kwamba uwanja sio mzuri na hivyo tulibadili kidogo aina ya uchezaji wetu kwa kucheza mipira mirefu na tulifanikiwa kufanya hilo.

"Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji na kiukweli imekuwa siku nzuri," alisema Aussems baada ya mchezo huo

Ushindi huo umepunguza tofauti ya pointi dhidi ya timu zailizo kileleni.

Simba imefikisha alama 42, alama nane nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 50, na alama 16 nyuma ya Yanga inayoongoza ligi ikiwa na alama 58

Hata hivyo Simba ina michezo saba pungufu dhidi ya Yanga na Azam FC

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’