Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo wakati mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara wakichuana na African Lyon
Simba itakuwa inatupa karata muhimu kusaka pointi tatu ugenini ili kuendelea kusogea kileleni mwa msimamo wa ligi
"Ni mchezo muhimu ambao tunahitaji kushinda ili tuzidi kwenda mbele zaidi. Kwa mashabiki tuliopo Arusha tujitokeze kuishangilia timu yetu," imesema taarifa ya Simba
Michezo minne ya ligi kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kupigwa leo kwenye viwanja mbalimbali

ADVERTISE HERE