Okwi azipigia hesabu pointi tatu Arusha

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Feb 2019
Okwi azipigia hesabu pointi tatu Arusha

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi amesema baada ya kumalizana na watani zao Yanga kwa ushindi wa bao 1-0, lengo lao ni kuhakikisha wanashinda michezo yote ya viporo ili kuweza kuwaondoa wapinzani wao kileleni

Okwi amesema katika mchezo wa kesho dhidi ya African Lyon na michezo mingine itakayofuata, hawapaswi kufanya makosa ili waweze kufikia malengo yao

"Tumemalizana na Yanga, kwa sasa hatuwafikirii tena, kilichobaki ni kupigania pointi katika michezo iliyobaki kuhakikisha tunamfikia mpinzani wetu, tunajua yupo juu yetu lakini tutapambana kumfikia," amesema Okwi.

"Hatuangalii idadi ya mechi za viporo tulizonazo, bali tunacheza mechi moja baada ya nyingine ili kutafuta pointi na kila mchezo kwetu tutapambana, lengo ni pointi tatu kama tulivyochukua kwa Yanga na huko kwingine tunazitaka"

Simba ina faida ya michezo nane dhidi ya Yanga inayoongoza ligi ikiwa na alama 58, alama 19 zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 39

Kimahesabu, Simba inaweza kuiondoa Yanga kileleni iwapo itashinda angalau michezo saba ya viporo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’