Beki Zana Coulibaly ameendelea kuwanyamazisha waliokuwa wakimkosoa baada ya jana kun'gara katika mchezo dhidi ya Yanga
Coulibaly ndiye aliyekuwa kiongozi wa mashambulizi ya Simba pembezoni, upande wake ukitumika zaidi
Aliweza kuwapa wakati mgumu walinzi wa Yanga hasa Abdallah Shaibu ambaye mara kwa mara alijikuta 'akiachwa kwenye mataa'
Hakuwa na mwanzo mzuri katika klabu ya Simba lakini sasa ameanza kuonyesha makali yake
Coulibaly pia 'alikiwasha' kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly mapema wiki hii ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kama ilivyokuwa jana dhidi ya wapinzani wao wa jadi
ADVERTISE HERE