Bao lake alilowafunga Yanga leo limemfanya Meddie Kagere afikishe mabao tisa, akiachwa mabao mawili tu na Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 11
Ikumbukwe Yanga imecheza michezo nane zaidi ya Simba. Kwa mwendo huu wa kutupia kila mechi, hakuna shaka kiatu cha dhahabu hakiwezi kupoteza njia
Mapema wiki hii Kagere pia alipeleka kilio nchini Misri akiwafunga Al Ahly bao pekee.
Mtengenezaji wa bao hilo alikuwa ni huyuhuyu John Bocco ambaye ameifanya tena kazi hiyo leo
Bocco amekuwa akikosolewa sana na baadhi ya mashabiki kuwa anakosa sana nafasi za wazi lakini nadhani umuhimu wake unaonekana zaidi katika michezo muhimu pia
ADVERTISE HERE