Kikosi cha Simba leo jioni kimejifua kwenye uwanja wa Boko Veterans yakiwa ni mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Februari 16 katika uwanja wa Taifa ukitarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni
Simba ilitinga uwanjani hapo majira ya saa kumi kasoro Alasiri
Morali ya wachezaji wa Simba iko juu na kikosi cha kocha Patrick Aussems kimeonyesha utayari kuelekea mchezo huo
Mashabiki wa Simba wametakiwa wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kesho kuwaunga mkono wapambanaji hao ambao wameahidi kuwapa furaha
ADVERTISE HERE