Mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye dimba la Taifa unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni kulingana na taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Mchezo huo namba 270 utachezeshwa na Hance Mabena ambaye atasaidiwa na waamuzi wasaidizi, Mohammed Mkono na Kassim Mpanga wakati Mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii

ADVERTISE HERE