Msemaji wa Yanga Dismas Ten ameingia matatizoni baada ya ktoa tuhuma ambazo zinailenga Simba kuwa hupulizia dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo timu pinzani
Ten alizitoa tuhuma hizo mapema jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amemtaka Ten athibitishe tuhuma zake kabla klabu haijamfikisha mbele ya vyombo vya Sheria ili akathibitishe
"Hili sio jambo la kupuuzwa na kwa kuwa Simba ndio iliomfunga Mwarabu na kwa kuwa tunacheza na hiyo klabu yake kesho,nadhani kuna haja na hoja ya huyu mtu kuthibitisha beyond reasonable doubt kuwa Simba inafanya mambo hayo," amesema Manara
"Tena uthibitisho huu uwe ktk vyombo vya kisheria"
"Tunaukubali utani ila sio tuhuma za kutuchafua. Angekuwa shabiki wa mtaani au mtandaoni tungepuuza ila kwa mtu mwenye dhamana ndani ya klabu ni lazma atoe uthibitisho"
"Simba ni klabu kubwa ni klabu inayoheshimika kote Afrika ni klabu yenye mamilioni ya wafuasi,hatutakubali kuchafuliwa kihuni huni na watu wasiojua maadili,miiko na kanuni za football"
"Tunamalizana nao kesho na baada ya hapo tutahitaji athibitishe hizi tuhuma
"Mningojee nikifa au nikiwa sipo katika nafasi hii, sitakubali na haitatokea mtu yoyote kuiharibu brand na image ya klabu yetu kwa kisingizio chochote kile"