Juuko atuliza presha ya mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Feb 2019
Juuko atuliza presha ya mashabiki Simba

Beki kisiki Mganda Juuko Murshid anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoikabili Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa kesho dimba la Taifa licha ya kuibua sintofahamu jana

Katika mazoezi ya jana, Juuko alifanya mazoezi ya peke yake sababu ikiwa ni majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly

Hata hivyo beki huyo asiye na maneno mengi amesema yalikuwa ni maumivu ya kawaida na atakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho

Aidha kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amethibitisha kuwa Juuko atakuwa sawa na hana wasiwasi atamtumia kwenye mchezo huo

Juuko amekuwa nguzo ya safu ya ulinzi ya Simba akishirikiana na Paschal Wawa 'Sultan' hasa baada ya kuumia Erasto Nyoni ambaye nae ameanza mazoezi mepesi

Nyoni hatarajiwi kucheza kesho kwani atahitaji muda zaidi kuimarisha mwili wake baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki tatu kutokana na majeraha ya goti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’