Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amebainisha kuwa katika mchezo wa kesho dhidi ya Yanga timu yake itaingia kwa lengo la kushambulia akitaka mabao ya haraka
Aussems ambaye hii itakuwa mara yake ya pili kukutana na Yanga, amesema hatarajii makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana kuwa yatajitokeza tena
Amesema safari hii anataka kuona wachezaji wake wanatumia nafasi watakazotengeneza kufunga mabao
"Hatutawadharau wapinzani wetu, lakini tunataka kushinda mchezo huo, " amesema
"Nimewaambia wachezaji wangu kuwa sitaki makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza yajirudie, ni lazima tutumie nafasi tunazotengeneza"
Aidha matokeo ya ushindi iliyopata Simba dhidi ya Al Ahly juzi, yameongeza mzuka wa kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara
Simba imeweka kambi jijini Dar es salaam ikiachana na utaratibu wa kutoka nje ya jiji. Iko katika moja ya Hotel maarufu iliyo pembezoni mwa bahari ya Hindi