Yanga hofu tupu kumkabili Mnyama kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Feb 2019
Yanga hofu tupu kumkabili Mnyama kesho

Hakuna anayeweza kubisha kuwa katika ligi ya hapa Tanzania ubora wa Simba umeziacha mbali sana timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ikiwemo Yanga ambayo mafanikio yao msimu huu yamechangiwa zaidi na bahati

Baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vigogo wa soka Barani Afrika Al Ahly, Simba itaingia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga ikiwa na morali kubwa

Aidha matokeo ya ushindi dhidi ya Al Ahly yameongeza hofu kwa wapinzani wao ambapo kocha Mwinyi Zahera  atakuwa anajiuliza ni vipi ataweza kuidhibiti timu iliyokiangusha kigogo cha soka barani Afrika siku chache zilizopita?

Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana lakini Yanga ilipaswa wamshukuru mlinda lango wake Beno Kakolanya ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo

Hata hivyo Kakolanya kwa sasa sio sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba hapo kesho baada ya kuondolewa kikosini na Zahera kufuatia mgomo aliofanya kudai stahiki zake

Kukosekana kwake ni sababu nyingine inayoongeza hofu kwa Yanga ambayo itamtegemea zaidi kinda Ramadhani Kabwili

Kwenye mchezo wa kesho Simba inatarajiwa kuendeleza pale ilipoishia katika mchezo dhidi ya Al Ahly.

Ni mchezo ambao Simba inahitaji kushinda ili kuongeza 'mzuka' wa kula viporo ili kuhakikisha ubingwa wa ligi kuu unabakia Msimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
20h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’