Kichuya awataka Okwi, Kagere, Bocco wamalize kazi Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Feb 2019
Kichuya awataka Okwi, Kagere, Bocco wamalize kazi Jumamosi

Mchezo wa keshokutwa kati ya Yanga na Simba utakaopigwa uwanja wa Taifa, Simba haitakuwa na kiungo wake mshambuliaji Shiza Kichuya ambaye ni wiki iliyopita tu alijiunga na Pharco Fc ya Misri na kutolewa kwa mkopo klabu ya ENPPI inayoshiriki ligi kuu nchini humo

Kichuya ameweka rekodi ya kipee katika michezo ya 'derby' akiwa amefunga kwenye michezo mitatu mfululizo

Lakini licha ya kuwa hayuko na Simba kwa sasa, Kichuya ameitakia kheri timu yake hiyo ya zamani ambayo ndiyo iliyompa nafasi ya kuonekana na baadae kumuuza nchini Misri

Kichuya amesema anaamini Simba ina nafasi ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo huku akiwataja John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi kuwa lazima watapeleka kilio Jangwani

Amesema hata hivyo mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na presha ya nje ya uwanja ambayo hupelekea hali kubwa ya ushindani

"Simba ina nafasi kubwa ya kushinda Jumamosi kutokana na ubora wa kikosi chake," amesema Kichuya

"Sisemi kama Yanga ni wabovu, lakini naamini Simba ina nafasi zaidi. Ina washambuliaji kama Bocco, Kagere na Okwi wanaoweza kuipa matokeo wakati wowote wakati Yanga inawategemea zaidi Makambo na Ajib"

"Muhimu Simba isiingie kwa presha, wacheze kwa makini naamini watashinda"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’