Kitambi kumsaidia Aussems Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Feb 2019
Kitambi kumsaidia Aussems Simba

Uongozi wa Simba umemalizana na kocha wa zamani wa Ndanda Fc Denis Kitambi ambaye tayari yuko nchini akisubiri kuanza rasmi kazi ya kumsaidia Patrick Aussems

Kitambi anatarajiwa kusaini mkataba wakati wowote kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma

Inaelezwa Kitambi alipendekezwa na Aussems mwenyewe baada ya kuridhishwa na wasifu wake akiamini anaweza kufanya nae kazi

Mbelgiji huyo alipewa majina ya makocha watano na kutakiwa apendekeze jana la kocha mmoja miongoni mwao.

Makocha hao ni pamoja na Etienne Ndayiragije wa KMC, Juma Mgunda wa Coastal Union, Selemani Matoka wa Lipuli Fc, Salum Mayanga (Mkurugenzi wa ufundi Mtibwa Sugar) na Denis Kitambi ambaye alikuwa akifundisha soka nchini Bangladesh

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Simba Crescentius Magori amesema wakati wowote wanatarajia kumsainisha Kitambi mkataba wa kuwa kocha msaidizi wa Simba

"Muda wowote kuanzia sasa tutamsainisha mkataba Kitambi ambao hatuwezi kusema ni wa muda gani kwa maana kila kitu kipo ndani ya mkataba wake na tumefanya hili baada ya kupendekezwa na kupitishwa na kocha wetu," amesema.

"Mkataba upo mezani kwetu na tumeshakubaliana na kumalizana kila kitu na Kitambi bado tu kusaini na kumtangaza kuwa rasmi anataanza kazi katika kikosi chetu kama kocha msaidizi akichukua nafasi ya Djuma ambaye aliacha nafasi hiyo wazi.

"Uongozi wa Simba unaheshimu maamuzi ya Aussems na kila ambalo atakuwa anahitaji wanamtekelezea haraka wawezavyo ili kuhakikisha yale malengo ambayo hata katika mkataba wake yapo yanatimia," amesema Magori.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’