Msimamo wa kundi D ligi ya mabingwa barani Afrika umegeuka baada ya michezo ya leo
Baada ya Simba kuichapa Al Ahly 1-0 katika mchezo wa mapema, JS Saoura nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vita Club katika mchezo uliopigwa nchini Algeria
Matokeo hayo yamelifanya kundi D liwe na ushindani mkali huku kila timu ikiwa na nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Al Ahly inaongoza kundi D ikiwa imejikusanyia alama saba ikifuatiwa na Simba yenye alama sita
JS Saoura imepanda mpaka nafasi ya tatu ikiwa imefikisha alama tano wakati AS Vita Club sasa inaburuza mkia ikiwa na alama nne
Michezo ya raundi ya tano inatarajiwa kupigwa March 09 ambapo Simba itasafiri kwenda nchini Algeria kuikabili JS Saoura wakati AS Vita Club itakuwa nyumbani ikichuana na Al Ahly