Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mbinu waliyoitumia kufanya mashambulizi mfululizo langoni kwa Al Ahly mwanzoni mwa mchezo ilipelekea walinzi wa timu hiyo kuwa na hofu.
Aussems amesema baada ya kuwa wamefanikiwa, Al Ahly walilazimika kucheza kwa kujihami na kuwapa Simba nafasi ya kutawala mchezo na kutengeneza nafasi zaidi
"Tulianza kwa kuwashambulia tangu mwanzo ili kuwaweka mabeki wao katika hofu"
"Bao tulilopata katika kipindi cha pili lilikuwa muhimu sana kwani liliongeza utulivu na kujiamini kwa wachezaji wetu," amesema Aussems
"Tulihitaji kushinda mchezo huu, tunashukuru tumefanikiwa. Nawapongeza wachezaji wangu kwa mafanukio haya, lakini pia nawashukuru mashabiki kwa kuja uwanjani kutuunga mkono"
Ushindi huo wa bao 1-0 umeweka hai matumaini ya Simba ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa sasa ikishika nafasi ya pili kundi D baada ya kufikisha alama sita