Umuhimu wa mashabiki kufurika uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Feb 2019
Umuhimu wa mashabiki kufurika uwanja wa Taifa leo

Imethibitishwa wingi wa mashabiki uwanjani huongeza hamasa na morali ya wachezaji kuwafanya wacheze kwa kujituma zaidi

Hii ndiyo sababu inayosema kuwa mashabiki ni wachezaji wa 12 uwanjani

Simba inao uwezo wa kuifunga Al Ahly leo, wingi wa mashabiki utachangia kwa kiasi kikubwa kuwezesha hili

Mashabiki watakaoingia uwanjani pia wameaswa wasikae kimya. Ushangiliaji unapaswa uendelee kwa muda wote wa mchezo

Matokeo ya ushindi leo yana maana kubwa kwa Simba na Tanzania pia

Kwa wale wasiofahamu, Simba ikifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa mwaka huu, msimu ujao idadi ya timu kutoka Tanzania zitakazoshiriki michuano hiyo zitaongezeka

Kwa muda mrefu Tanzania tumepewa nafasi mbili tu kwenye michuano ya CAF, moja ligi ya mabingwa na nyingine kombe la Shirikisho. Hii ni kutokana na timu zetu kutofika mbali katika michuano hiyo

Kuna nchi zimepewa hadi nafasi nne, Misri ikiwa mojawapo kutokana na mafanikio ya timu zake katika michuano ya kila mwaka

Hata Zambia mwaka huu wameingiza timu mbili kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kutokana na mafanikio ya ZESCO United misimu miwili iliyopita

Watanzania wote wameaswa kuiunga mkono Simba katika mchezo wa leo kwani mafanikio yake ni mafanikio ya Tanzania

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
28m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
18h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
18h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
21h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’