Simba vs Al Ahly, kila la kheri Mnyama

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Feb 2019
Simba vs Al Ahly, kila la kheri Mnyama

Leo mabingwa wa Tanzania Bara Simba wanashuka katika dimba la Taifa kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa kundi D, raundi ya nne michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni mchezo ambao utabainisha hatma ya Simba kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems pamoja na wachezaji wameahidi kupambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha wanachukua alama zote tatu dhidi ya Al Ahly leo.

Mashabiki kutoka kila pembe ya jiji la Dar es salaam na mikoa ya jirani wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuwapa sapoti wapambanaji wetu ambao watakuwa wakiiwakilisha Tanzania katika mchezo huo

Kuna umuhimu mkubwa kwa uwanja wa Taifa leo kufurika na kuzizima kwa kelele za mashabiki kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo mpaka dakika ya 90

Hakuna jambo lisilowezekana, kama timu nyingi katika michuano hii zinashinda michezo ya nyumbani kwa nini Simba isiweze?

Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata katika mchezo wa kwanza dhidi ya JS Saoura unathibitisha uwezo wa Simba inapocheza uwanja wa Taifa

JS Saoura walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya hii Al Ahly katika mchezo uliopigwa nchini Algeria. Wanafungika, bila shaka leo ni zamu yao kupoteza mchezo dhidi ya Mnyama

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
6h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’