Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema hakuna mabadiliko ya muda wa mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Taifa
Kufuata taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mchezo huo utapigwa saa moja jioni, Manara amesisitiza kuwa muda ni ule ule yaani saa kumi kamili Alasiri
Amewataka mashabiki wa Simba kununua tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu wa aina yoyote unaoweza kujitokeza hapo kesho
Leo uongozi wa Simba leo ulikutana kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao ushindi ndio matokeo yanayohitajika zaidi ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali kwa Simba
ADVERTISE HERE