Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly
Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari leo, Tshabalala amesema wanayo kila sababu ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho hasa ikizingatiwa walipoteza mchezo wa ugenini
"Kesho tuna mchezo muhimu sana. Tumejipanga kufanya vizuri. Tulipoteza mchezo wa ugenini kwa goli nyingi lakini alama ni zilezile tatu"
"Nasi tumejipanga kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo wa kesho," amesema Tshabalala
"Ukiangalia mwenendo wa michuano hii, kila timu imekuwa ikifanya vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani. Nasi kesho tuko nyumbani, tumedhamiria kutumia vyema uwanja wa nyumbani"
Ushindi kwa Simba kwenye mchezo wa kesho utafufua matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo ikihitaji pia kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita Club bila ya kujali matokeo ya mchezo wake dhidi ya JS Saoura
Β