Wachezaji Simba waapa kuwamaliza Al Ahly kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Feb 2019
Wachezaji Simba waapa kuwamaliza Al Ahly kesho

Mwishoni mwa wiki Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo aliwataka wachezaji wa Simba kutambua thamani ya jezi ya klabu hiyo.

Mo alitamka bayana kuwa wachezaji wavivu ambao hawajitumi na wasio na nidhamu hawatakuwa na nafasi msimu ujao

Mo alibainisha kuwa Simba imedhamiria kuachana na wachezaji wasiokuwa na faida kwa timu hiyo mwishoni mwa msimu. Lakini kwa sasa bado wana nafasi ya kujisahihisha na kuushawishi uongozi wa timu hiyo kuendelea kuwa nao

Kauli hiyo ya Mo imewaingia wachezaji wa Simba ambao kesho wameapa kushinda mchezo dhidi ya Al Ahly

Nahodha wa Simba John Bocco amesema mchezo wa kesho una umuhimu wa kipekee kwao wachezaji na Wana Msimbazi wote

"Mchezo dhidi ya Al Ahly una umuhimu wa kipekee kwetu. Tunahitaji kushinda ili tuwe na nafasi ya kutinga hatua inayofuata," amesema Bocco

"Hatukufanya vizuri kwenye michezo miwili iliyopita lakini kesho tuna nafasi ya kusahihisha makosa yetu. Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani, hatutawaangusha"

Mchezo dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Taifa, unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni

Wengi walitamani mchezo huo upigwe mapema zaidi hata hivyo Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeweka msisitizo kwa michezo yote kuanza kuda wa saa kumi na kuendelea

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’