Al Ahly ilifaa tuwachezeshe saa nane mchana - Rage

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Feb 2019
Al Ahly ilifaa tuwachezeshe saa nane mchana - Rage

Miamba ya soka Misri Al Ahly imewasili nchini leo saa 10 alfajiri wakitokea Cairo, Misri tayari kwa mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa keshokutwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, lakini Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage amesema ilifaa wachezeshwe saa 8:00 jua kali.

Wachezaji wa Al Ahly wakiongozwa na kocha wao raia wa Uruguay, Lassarti waliondoka jana usiku saa 4:30 na walitarajiwa kufika saa 10:00 alfajiri tayari kwa mchezo huo.

Al Ahly ndio inayoongoza kundio hilo la D ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na AS Vita na Simba na JSS zinafuatia.

Endapo Simba itaing’ang’ania timu hiyo, itafikisha pointi sita na kushika nafasi ya pili, lakini pia itategemea matokeo ya mechi ya marudiano ya JSS na AS Vita kule Algeria.Simba ilifungwa mabao 5-0 wakati timu hizo zilitoka sare ya 2-2 mjini Kinshasa.

Rage alisema kuwa mbinu moja wapo ya kuwachosha Waarabu ilikuwa kuwachezesha mchana wa jua kali.

“Kule kwao hali ya hewa ni baridi sana na usiku ndio kuna baridi kali, na ndio maana wakawapeleka Simba kwenye baridi, inawezekana na ndicho kiliwashinda kucheza kutokana na hewa kuwa nzito, sasa ili kuwachosha na joto, mechi ingepigwa saa 8 au 9 kwenye jua kali,” alisema Rage.

Rage aliyewahi kuongoza Simba aliwataka wachezaji wa timu hiyo kujituma na kusimama kila mmoja na mtu wake bila kuwapa nafasi.

“Simba wanajiachia mno, inatakiwa kuwabana na kutowapa nafasi, kila mmoja acheze na mtu wake ili kuwabana,” alisema Rage.

Akizungumzia mchezo huo, nahodha msaidizi wa timu hiyo na beki wa pembeni wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alisema watakomaa kuhakikisha wanavuna pointi zote tatu dhidi ya Al Ahly ya Misri ingawa amekiri kazi itakuwepo.

Tshabakaka alisema wameendelea kufanyia kazi upungufu katika kikosi chao ikiwemo safu ya ulinzi na naamini katika mchezo huo hawataruhusu bao.

“Kila mara tumeendelea kuimarika na kupunguza makosa na ndio maana hata kwenye mchezo wa Mwadui hatukuruhusu bao hivyo tutapambana mchezo dhidi ya Al Ahly tufanye hivyo hivyo.

"Utakuwa mchezo mgumu kwani wapinzani wetu ni moja ya timu kubwa na bora Afrika hivyo haitakuwa kazi rahisi kuwafunga lakini tuko nyumbani na mcheza kwao hutunzwa hivyo naamini hiyo mechi tunashinda”alisema Tshabalala.

Tshabalala amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kujaza uwanjani kwani uwepo wao utawapa nguvu ya kupambana zaidi.

"Tunashukuru mashabiki wetu wamekuwa wakitusapoti katika hali zote iwe tumeshinda au tumepoteza hivyo nawaomba waendelee kutuunga mkono kwa kujaa uwanjani na kutupa sapoti na sisi hatutawaangusha,” alisema.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’