Ajira ya Manara iko salama - Nkwabi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Feb 2019
Ajira ya Manara iko salama - Nkwabi

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Swedi Nkabi amesema Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amekuwa na mchango mkubwa na hawana sababu ya kumuondoa katika wadhifa wake

Baada ya juzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' kuzungumza na waandishi wa habari tofauti na ilivyozoeleka kwa kazi hiyo kufanywa na Manara, ziliibuka taarifa kuwa uongozi wa Simba ulikuwa mbioni kufanya mabadiliko kwa nafasi ya Manara

Nkwabi amesema Manara ataendelea kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba.

Kilichofanyika juzi ni utaratibu wa kawaida.

Kulikuwa na umuhimu kwa Mo kuzungumza na Wana Msimbazi kuelekea mchezo dhidi ya Al Ahly na pia kauli yake ilikuwa muhimu hasa baada ya klabu kukumbwa na wakati mgumu kufuatia kupoteza michezo miwili ya ligi ya mabingwa dhidi ya Vita Club na Al Ahly

"Haji Manara bado ni msemaji wa Simba, ukiangalia hata jana kupitia Instagram yake aliandika kuhusiana na masuala mbalimbali ya klabu pamoja na kwenye ukurasa rasmi wa timu, si kweli kuwa ataondoshwa" amesema Nkwabi

Wakati huo huo, Manara amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya Al Ahly

Amesema licha ya kutambua kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini mashabiki wanayo nafasi ya kuchangia matokeo mazuri kwa Simba

"Unaanzaje kukosa mechi ya kihistoria kati ya Mabingwa wa muda wote wa Afrika dhidi ya Mabingwa wa muda wote wa Afrika Mashariki na ya kati?," ameandika Manara katika ukurasa wake wa Instagram

"Ndio, maara ya mwisho miamba hii kukutana Tanzania ni Mwaka 1985 ( miaka 33 iliopita) kule CCM kirumba Mwanza

"Huu ni mchezo muhimu utakayotupa mwelekeo wetu wa baadae katika makundi

"Hakuna shaka utakuwa mgumu lakini washabiki wanayo nafasi kubwa ya kutupa matokeo chanya

"Kwa msiojua Ahly ya wakati huo ilikuwa zaidi ya balaa, huku ikiwa na nyota waliotingisha Afrika akiwemo Mohammed El khatib 'Bibo', Rabii Yassin, Alaa Maihoub, Ahmed Shouber, Majid Abdelghan na mawaria wengine ila walikufa 2-1 kwa Simba. Kwa nini isiwe Jumanne hii?

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’