Timu ya Al Ahly imewasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Alfajiri ya leo Jumapili tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba utakaopigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Taifa
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na Wana Msimbazi unatarajiwa kupigwa saa kumi kamili jioni
Inaelezwa awali uongozi wa Simba ulipanga mchezo huo upigwe saa nane mchana lakini Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) lilipinga muda huo
Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua katika uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo huo ambao Simba inahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali.
ADVERTISE HERE