Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewataka mashabiki kusahau matokeo mabaya ya michezo iliyopita ya ligi ya mabingwa na kujitokeza kwa wingi siku ya Jumanne kuiunga mkono Simba itakapokuwa ikichuana na Al Ahly
Mo amewataka mashabiki kuonyesha upendo wao kwa Simba kwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega wakati wa raha na shida
"Ni rahisi kujitokeza na kuchukua sifa iwapo Simba itashinda, lakini mashabiki wa kweli ni wale ambao wanajirudi na kushangilia Simba pindi inapopita katika kipindi kigumu," amesema Mo
"Mashabiki wa kweli wanakuwepo wakati mzuri na wakati mbaya"
Jumanne Simba itachuana na Al Ahly katika mchezo ambao inahitaji matokeo ya ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Simba imeweka rekodi nzuri ya kushinda michezo yote ya ligi ya mabingwa iliyocheza kwenye dimba la Taifa mpaka sasa msimu huu.
Pamoja na sapoti ya mashabiki wake, Simba imedhamiria kuendeleza rekodi hiyo ya ushindi siku ya Jumanne itakapoikabili Al Ahly.