Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ndiye Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Simba, amesema bado hajakata tamaa ya kuiongoza Simba kutwaa ubingwa Afrika
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mo amesema ana dhamira ya kuijenga Simba imara zaidi ikiwemo kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka
Amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumanne ijayo kuipa sapoti Simba itakapochuana na Al Ahly kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ambapo kiingilio kitakuwa Tsh 2000/- tu
Amesema Simba inahitaji kuungwa mkono na mashabiki wake na hata wale wasio wa Simba ili kuhakikisha inashinda mchezo huo kwani mafanikio ya Simba katika michuano hiyo yatasaidia kuongezwa kwa timu zitakazoshiriki awamu zijazo
Amesema Simba ilipoteza mechi za ugenini dhidi ya timu kubwa zenye bajeti kubwa mfano Al Ahly yenye mchezaji mmoja ambaye thamani yake ni billion 10 hivyo wapo juu kiuchumi kulinganisha na Simba ambayo ndio imeanza mabadiliko hivi karibuni.
Amesema uwingi wa mataji Al Ahly ni sawa na klabu ya Real Madrid
Pia Mo amewataka wachezaji wa Simba kutambua thamani ya klabu hiyo na kuhakikisha wanaipigania kikamilifu
Amesema Simba haitaendelea kuwavumilia wachezaji ambao hawana nidhamu.
Ametahadharisha wachezaji hao kuwa hawataongezewa mikataba mingine pale mikataba yao itakapomalizika kama wataendelea kuwa watovu wa nidhamu
Mo amesema Simba imedhamiria kutetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu ili iweze kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Kuhusu ujenzi wa uwanja wa Bunju Mo amesema unaenda vizuri na wanakamilisha taratibu za kiserikali ili kuweza kupewa nyasi kwa ajili ya kuzitandika iliΒ mwezi ujao uwanja huo uanze kutumika kwa mazoezi.
Kuhusu usajili wa Kimataifa kwa wakati huu Mo amesema si rahisi kupata mchezaji mwenye ubora maana wenye ubora ndio hao walishiriki michuano ya CAF ambapo kanuni haziruhusu kuchezea timu zaidi ya moja kwa msimu mmoja.
Amesema katika kipindi kijacho Simba haitaleta wachezaji wa majaribio, itanunua moja kwa moja baada ya kutambua ubora wao