Aussems ataka ushindi dhidi ya Mwadui Fc leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Feb 2019
Aussems ataka ushindi dhidi ya Mwadui Fc leo

Licha ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa siku moja tangu watoke nchini Misri, kikosi cha Simba leo kitashuka katika uwanja wa Taifa kuikabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Simba ilifanya mazoezi ikiwa na kikosi chake kamili jana baada ya wachezaji wa timu hiyo kurejea kutoka Misri kwa awamu tofauti kutokana na changamoto ya usafiri

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanahitaji kushinda mchezo wa leo

Amesema ni lazima wachezaji wake wajitume kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo utakaoanza saa moja usiku

Aussems amesema licha ya timu yake kukabiliwa na ratiba ngumu, wanapaswa kufanya vizuri katika michezo yao ili kutimiza lengo la kutetea ubingwa

"Huu ni mchezo muhimu sana kwetu unajua tuna lengo la kutetea ubingwa na jana ndiyo siku pekee tuliyoweza kufanya mazoezi kwa pamoja tangu turudi nchini kutokana na utofauti wa safari ya kurejea nchini tukitokea Misri," amesema Aussems."

"Tuna ratiba ngumu katika mechi zetu ndani ya wiki mbili zijazo ukiangalia tunatakiwa kucheza mechi sita ndani ya siku 18 hii ni ngumu lakini hakuna namna ni lazima tupambane"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’