Beki kiraka wa Simba Erasto Nyoni leo alifika uwanja wa Boko Veterans kushuhudia mazoezi ya kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mwadui Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Taifa saa moja jioni

Nyoni aliumia wakati akiitumikia Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na alipewa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurejea rasmi dimbani kuanza mazoezi
Mkongwe huyo ambaye pengo lake lilionekana sana kwenye michezo miwili ya ligi ya mabingwa dhidi ya Vita na Al Ahly, anakaribia kurejea dimbani baada ya kupona majeraha yake
ADVERTISE HERE