Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema usajili wa mshambuliaji Vitalis Mayanga aliyesajiliwa na Simba kutoka Ndanda Fc kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa, utakuwa na masaada kwa timu hiyo
Aussems amesema ameridhishwa na uwezo wa Mayanga, anaamini ataweza kuziba pengo la Shiza Kichuya aliyeuzwa Misri
Amesema Mayanga anahitaji muda kufanya mazoezi na kikosi cha Simba ili azoee utamaduni wa timu hiyo kabla hajaanza kumtumia
"Nimeukubali usajili wa Mayanga, ni mchezaji mzuri ambaye naamini ataendana na kasi ya timu yetu, tumemwachia Kichuya kuondoka, hivyo ilikuwa lazima kupata mchezaji mwingine mbadala," alisema Aussems.
Simba inajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc utakaopigwa uwanja wa Taifa kesho kabla ya kuwavaa Al Ahly kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne ijayo